السبت، 27 أغسطس 2016

UTUKUFU WA SIKU 10 NA MAMBO GANI YA KUFANYA
Siku bora kabisa katika mwaka mzima ni Siku hizi 10 za mwanzo wa mwezi wa DHULHIJJAH.
Naam ni bora hata kuliko Ramad...han!
Masiku(wingi wa usiku) kumi ya mwisho ya Ramadhan ni bora lakini michana yake si bora kuliko siku hizi.
Mungu s.w.t. ameapa kwa siku hizi akasema :
والفجر ¤ و ليال عشر ¤
Na Mtukufu s.w.t. hafanyi kiapo ispokuwa kwa kitukufu.

Na Mtume ﷺ katika kutuonyesha utukufu wa hizi siku akasema.
أفضل أيام الدنيا أيام العشر
Siku bora zaidi za dunia ni siku kumi (hizi za dhulhijjah)
[Imepokewa na Ibn Hibban]

Amesema Abu Uthman Annahdiy 'Wema waliotanguliya walikuwa wakitukuza siku 10 tatu:
Siku 10 za mwanzo wa Dhulhijjah
Siku 10 za mwanzo wa Muharram
Siku 10 za mwisho wa Ramadhan '

amesema Ibn Hajar katika fathul baari:
Siku hizi 10 za dhulhijjah ni tukufu kwa sababu ndani yake zimekusanyika fadhila mama za ibada kama swala, kufunga,kuchinja na swadaka , hajj....ambazo hazikusanyiki katika mwezi mwingine

MAMBO GANI TUFANYE KATIKA SIKU HIZI ???
kutoka kwa Ibn Abbas Mtume ﷺ amesema " hakuna siku ambazo amali njema ndani yake ni bora kuliko katika siku 10 (za dhulhijjah) "
[Imepokewa na Bukhari]

1.Swaum
Imepokewa kutoka kwa wake za Mtume ﷺ kuwa Mtume ﷺ alikuwa akifunga siku tisa za mwanzo wa Dhulhijjah.
[Imepokewa na AbuDaud na Annasai]

Na kutoka kwa Hafswa radhiya Allahu anhaa mke wa Mtume ﷺ amesema :
Mtume ﷺ alikuwa hawachi kufunga Ashuraa na siku 10 za dhulhijjah na siku 3 katika kila mwezi.

Na khaswa siku ya Tisa siku ya Arafa ambayo kwa kuifunga unasamehewa madhambi ya miaka miwili.
2.Hajj
Tunajua kuwa hizi ndizo siku za Hajj na Mtume ﷺ amesema
"Hajj mabrur haina malipo ispokuwa jannah"
[Imepokewa na Bukhari na Muslim]

3. Kukithirisha kumtaja Allah
Allah s.w.t amesema
(ويذكروا اسم الله في أيام معلومات على ما رزقهم من بهيمة الأنعام) [الحج:28]
Na Mtume ﷺ amesema
" " hakuna siku ambazo amali njema ndani yake ni tukufu na zinapendekeza zaidi kuliko katika siku 10 (za dhulhijjah) , basi fanyeni wingi katika Takbir na Tahlil na Tahmid" [imepokewa na Imam Ahmad]
yaani semeni sana Alhamdulillah, Allahu akbar na Laa ilaaha illa Llah.

4.kuchinja katika siku za 10 , 11 ,12 na 13
Mtume ﷺ amesema
(( ما عمل ابن آدم يوم النحر عملاً أحب إلى الله تعالى من إراقة دم»
" hajafanya binadamu Amali bora zaidi katika siku ya kumi (yawmu nnahr) kama amali ya kuchinja.."

Na katika yanayopendekezwa kwa anaetaka kuchinja siku ya kumi ni asikate kucha zake wala nywele zake kwanzia siku ya kwanza kama Mtume ﷺ alivyoagiza
إذا دخلت العشر، وأراد أحدكم أن يضحي، فلا يمس من شعره وبشره شيئًا»
[Imepokewa na Imam Muslim]

Na kila aina ya ibada Tufanyeni sana kama Qur'an, kumswalia Mtume ﷺ , kuunga undugu , kutendea wema majirani na maskini. ..n.k.
KWAHIVYO NI SIKU TUKUFU SANA
*NA KAMA HUSHINDANI NA WEMA KATIKA KUONGEZA MEMA BASI USISHINDWE NA WAPUNGUFU KATIKA KULETA ISTIGHFAAR . NA NI HASARA ILIYOJE KWA ANAEKUSUDIYA KUFANYA MADHAMBI KATIKA SIKU HIZI TUKUFU*





ليست هناك تعليقات:

إرسال تعليق