الاثنين، 28 نوفمبر 2016

MAZINGATIO NI KUFATA HAKI NA SIO KUFATA WENGI HATA KAMA WAKO KWENYE MAKOSA
- Miongoni mwa sababu za kupinda ni kuwafuata wengi waliofanya vibaya na kutumia hoja kwamba watu wengi wako katika hayo.

Vijana wengi wanafanya kitu, wanabuni maoni au fikira kwa sababu ya kuona watu wengi wako katika jambo hilo, vijana wengi katika jambo hilo au kwa sababu anaona watu wengi katika jambo hilo. Allaah (´Azza wa Jall) anasema:
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
"Kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza na njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu na hawakuwa ila wenye kubuni uongo." 06:116
Mja wa Allaah! Ukiwatii wengi waliyoko juu ya ardhi basi tambua kuwa watakupotosha kutoka katika njia ya Allaah. Alama ya hilo ni kuwa hawafuati uongofu wala dalili ya wazi. Kinyume chake wanafuata dhana, maoni, fikira, kanuni za uzushi zilizoundwa na wakati huo huo zikawa zinapingana na Qur-aan na Sunnah. Allaah (´Azza wa Jall) anasema tena:
وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ
"Wengi wa watu hawatoamini japokuwa utafanya bidii." (12:103)
Mzungumzaji: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
Chanzo: Inhiraaf-ush-Shabaab
Tarjama:



 

ليست هناك تعليقات:

إرسال تعليق